• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

MKURUGENZI NYASA AWATAKA WATUMISHI KUWAJALI WANANCHI

Posted on: June 25th, 2019

Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Nyasa, ndugu Jimson Mhagama, amewataka Watumishi wa Umma wilayani Nyasa, kutoa Huduma Bora kwa wananchi na wateja wao ili kuondoa changamoto mbalimbali katika jamii wanazo ziongoza.

Aliyasema hayo hivi karibuni akiwa katika katika ukumbi wa shule ya Sekondari ya Tingi, Kata ya Tingi, Tarafa ya Mpepo wakati akifungua maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2019. Maadhimisho haya huadhimishwa barani Afrika kila mwaka kuanzia Juni 18 hadi 23 ikiwa ni matukio katika kalenda ya Umoja wa Afrika (AU) kwa lengo la kuboresha huduma mbalimbali zinazotolewa katika Utumishi wa Umma.

Bwana Mhagama alifafanua kuwa, Watumishi wa Umma wanatakiwa kutoa huduma bora kwa wateja wao ili kujenga uaminifu na imani kubwa kwa wateja wao wanaofika katika ofisi za umma. Amesisitiza kuwa ubora wa huduma, uwatamanishe kurejea katika ofisi ya umma kwa huduma nyingine.

Aliongeza kuwa, ni aibu katika utumishi wa umma kutokuwa na huduma nzuri kwa kuwa wananchi wanakuwa hawana imani na utendaji wa Serikali yao. Aliwaagiza watumishi kuwa Wiki ya Utumishi wa Umma isaidie watumishi kukutana na kujua changamoto zinazowakabili.

“Nichukue fursa hii kuwaagizeni watumishi wenzangu katika wiki hii ya maadhimisho ya Utumishi wa Umma itukumbushe kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kuondoa changamoto mbalimbali zinazoikumba jamii na tuhudumie wananchi wetu kwa lugha nzuri na za upendo ili hata mtu awe na hamu ya kurudi tena katika ofisi yako akiwa na shida”. Alisema ndugu Mhagama.

Aidha katika hatua nyingine aliwa agiza watendaji wa kata na Vijiji kuendelea kutekeleza majukumu mbalimbali na kuachana na siasa kwa kuwa jamii inahitaji miundombinu ya shule, zahanati na Vituo vya Afya viendelee kujengwa bila kusimama na pale wanapo kwama waende katika Ofisi ya Mkurugenzi ili wapate ushauri zaidi.

Kwa upande wao watumishi walimshukuru Mkurugenzi kwa kuweza kukutana na watumishi hao na kumweleza kuwa watazingatia maagizo yote yaliyo tolewa na kutoa pongezi kwa Mkurugezi kwa kuwalipa stahiki zao kwa wakati hivyo kuwa morali ya kufanya kazi kwa juhudi.

“Tunachukua Fursa hii kukupongeza sana Mkurugenzi kwa kutupatia nauli kabla hatujaanza likizo huwa tunalipwa kabisa na stahiki zetu tunapata kwa wakati hivyo hatutakuangusha tutafanya kiazi kwa juhudi na nyasa itakuwa juu kwa utendaji makini miaka yote.” Alisema Mwalimu Meshak Mwadisa.

Maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma wilayani Nyasa yameadhimishwa kwa Mwajiri na Wakuu wa Idara kukutana na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili na kuzipa majibu, kukutana na wateja wao wanao wahudumia, na kufanya shughuli mbalimali za kijamii katika Hospitali ya Mbamba-Bay, wilayani hapa.

Announcements

  • TANGAZO LA KAZI YA MAFUNDI KWA AJILI YA HUDUMA YA UJENZI WA MAJENGO YA CHUO CHA VETA WILAYA YA NYASA. September 16, 2019
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI VILIVYOMO KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA NYASA September 13, 2019
  • Standard Four National Examination Results 2017 January 16, 2018
  • TANGAZO LA KULIPIA KODI YA ARDHI May 22, 2018
  • View All

Latest News

  • MAAFISA KILIMO NA VIONGOZI WA VYAMA VYA USHIRIKA WAJENGEWA UWEZO,NYASA NA MBINGA

    December 06, 2019
  • GIZA LASABABISHA KUAHIRISHA MCHEZO

    December 01, 2019
  • WILAYA YA NYASA YAADHIMISHA SIKU YA UKIMWI DUNIANI

    December 01, 2019
  • HALMASHAURI YAKAMILISHA KUWAAPISHA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA

    December 01, 2019
  • View All

Video

KUELEKEA TAMASHA LA UTALII 2019 WILAYANI NYASA
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.