• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

DED Nyasa awataka maafisa maendeleo kuwahamasisha wananchi kuchukua mikopo

Posted on: October 28th, 2024

Mkurugenzi wa Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Bw. Khalid Khalif amezitaka Kamati za huduma za mikopo ngazi ya kata  kusimamia suala zima la utoaji wa mikopo,  kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, kuanzia hatua ya uundaji wa vikundi sambamba na uibuaji wa miradi pamoja na kufuatilia miradi inayoenda kutekelezwa ili iweze kuleta tija katika kufanikisha dhana inayotarajiwa ya kuwainua kiuchumi.

Ameyasema hayo hivi karibuni katika mafunzo ya kuwajengea uwezo kamati hizo ili ziweze kutekeleza kazi zake kikamilifu

“Utoaji wa mikopo hii ni utekelezaji wa sera, mikakati na mipango ya taifa katika kupunguza umaskini, kwahiyo tunapoenda kutoa mikopo hii tukalenge katika kupunguza umaskini na si vinginevyo”,

Kupitia mafunzo haya wajumbe wa kamati hizo wamepitishwa katika muongozo na kanuni za utengaji, utoaji na usimamizi wa mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika mamlaka za serikali za mitaa ya mwaka 2024.

Akifafanua juu ya muongozo na kanuni hizo, Bi Stamil ngongi ambae ni Mratibu wa mikopo kwa vikundi Wilayani hapa, amesema kuwa, zoezi la utoaji wa mikopo kwa vikundi litafanyika kielektroniki kupitia mfumo wa maombi ya mikopo na kwamba kikundi hakitaruhusiwa kuomba mkopo mpya kama kina deni la zamani.

Aidha Bi Stamil amefafanua zaidi kwa kusema kuwa kutakuwa na kamati za utoaji wa mikopo kwa ngazi za mkoa, wilaya na kata na kwamba utengaji, utoaji na urejeshaji wa mikopo utafanyika kwa utaratibu wa 4;4;2 kwa maana ya kuwa asilimia nne kwa wanawake, asilimia nne kwa vijana na asilimia mbili kwa watu wenye ulemavu

Akifunga mafunzo Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mhe. Peres Magiri  amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii kuwahamasisha wananchi ili waombe mikopo ya asilimia 10 kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Kamati ya huduma za mikopo ngazi ya kata inaundwa na mtendaji wa kata, afisa maendeleo ya jamii wa kata, afisa ustawi wa jamii, afisa elimu kata, maafisa ugani wa kata, watendaji wa mitaa ya kata husika pamoja na polisi kata.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • UTEKELEZAJI KAMPENI YA CHANJO YA MIFUGO YAANZA NYASA

    July 12, 2025
  • MAKUNDI SOGOZI YA WHATSAAP YAPASWA KUJADILI MAENDELEO

    July 12, 2025
  • DC MAGIRI AZINDUA RASMI BODI YA MAJI WILAYA YA NYASA

    July 12, 2025
  • DKT.SAMIA AMWAGA TENA MAMILIONI YA MIRADI NYASA

    July 10, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.