• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

Halmashauri ya Nyasa yapata Hati safi,Mkuu wa Mkoa Ibuge aipongeza Nyasa kwa Mambo 3

Posted on: June 28th, 2022

 Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, imepata hati safi kutokana na ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa Fedha 2020/2021.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ameipongeza Halmashauri ya Nyasa kwa kufanikiwa kupata hati safi, Kutoa Mikopo kwa makundi maalum ya Vijana, walemavu na Wanawake na Ukusanyaji mapato ya ndani kwa asilimia 94.

Akizungumza katika Kikao cha Baraza la Madiwani La kujadili majibu ya hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Kepten John Komba Mbamba  bay Wilayani Hapa, Ibuge ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kuweza kukusanya mapato ya ndani kwa asilimia 94 Kutoa Mikopo ya Vijana walemavu na Wanawake kwa asilimia 100 na kupata Hati safi.

“nichukue fursa hii kuwashukuru Viongozi na wananchi wa Wilaya ya Nyasa kwa ushirikiano wenu wa kuhakikisha mnapata hati safi,ukusanyaji wa mapato ya ndani wa asilimia 94, na kutoa mikopo kwa makudni maalum kwa asilimia 100.

Aidha ameitaka Halmashauri ya Nyasa kuendeleza Mafanikio haya kwa kuboresha zaidi kwa mwaka huu wa fedha kwa kuzuia hoja badala ya kujibu Hoja.

Katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa ameagiza Halmashauri ya Nyasa kuhakikisha hoja zote zilizosalia zifungwe na kuzuia kujirudia kwa hoja na kwamba wakuu wa Idara washiriki kikamilifu kuandaa majibu ya hoja na utekelezaji wa mapendekezo ya CAG.

Balozi Ibuge ameagiza Halmashauri ichukue mapema hatua za kinidhamu kwa watumishi wanaozalisha hoja,na  kudhibiti upotevu wa mapato katika Halmashauri.

 Pia ameagiza Halmashauri kusimamia kikamilifu mfuko wa Bima ya Afya na Bima ya Afya iliyoboreshwa ili kila mwananchi aweze kujiunga ikiwa ni Pamoja na kufuatilia malipo yake kwenye vituo vya afya na zahanati.

Aidha ametoa wito kwa wananchi wa Wilaya ya Nyasa, kUhamasika kuhesabiwa Augosti 23 ili kupata idadi kamili ya watu itakayoisaidia Serikali kupanga mipango ya Maendeleo.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Mh. Wayariki Kikasi ameahidi maagizo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa yatafanyiwa kazi kikamilifu ili kujiletea maendeleo.

Imeandaliwa na Netho Sichali

Afisa Habari Wilaya ya Nyasa

Announcements

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI WILAYA YA NYASA April 18, 2023
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • TANGAZO la nafasi ya kazi February 03, 2023
  • View All

Latest News

  • Mhandisi Stella Manyanya yatatua kero ya wanafunzi kutembea km 30 kufuata shule ya Sekondari

    June 07, 2023
  • Tunaimani na Serikali, wananchi wa Kata ya Mtipwili na Chiwanda

    June 07, 2023
  • Dc Nyasa atembelea miradi ya Boost awataka mafundi kukamilisha Kwa wakati na ubora

    June 05, 2023
  • Mbunge Manyanya aridhishwa na Kasi ya ukuaji wa Utalii Wilayani Nyasa

    June 05, 2023
  • View All

Video

NYASA yampongeza Rais SAMIA jengo jipya la Utawala
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.