• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

HALMASHAURI YA NYASA YASHUSHA NEEMA KWA VIKUNDI 3 KATA YA LIPINGO

Posted on: August 19th, 2018

Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa leo imegawa mbolea mifuko 122 yenye thamani ya Tsh. 6,295,200/= kwa vikundi vya kilimo cha umwagiliaji vya akina Mama na Vijana wa kata ya Lipingo kwa ajili ya kuwawezesha kiuchumi ili kuinua kipato cha wakulima wa kata hiyo.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa ambaye ni Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika Ndg. Morton A. Msowoya amegawa mbolea hiyo leo katika Ofisi  ya Afisa Mtendaji Kata ya Lipingo kwa kuwataka wakulima hao kutumia mbolea hiyo kwa malengo ya kuweka kwenye mpunga wa kilimo cha umwagiliaji kama ilivyopangwa.

Kaimu Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa Halmashauri imeona  juhudi za serikali ya awamu ya tano kwa sehemu ya asilimia kumi ya mapato yake kupelekwa kwenye vikundi vya akina mama na vijana, leo hii Halmashauri imetekeleza agizo la Serikali kwa kuwaletea  mbolea mifuko 122 ya Urea na CAN ili kuboresha maisha ya Vijana na akina Mama wa vikundi vitatu vya Kata hii ya Lipingo

Akavitaja vikundi vinavyopewa mbolea hizo ni Mamanilee kikundi cha akina Mama kinachotoka Kijiji cha Lundo, Kikundi cha vijana cha Mwongozo kutoka KIjiji cha Lundo na Upendo Kikundi cha akina mama toka kijiji cha Ngindo vyote Kata ya Lipingo Wilayani hapa.

Akaongeza kuwa nimeiona mbolea na nimekagua ni nzuri na iko salama hivyo inatakiwa iende mashambani ili ikarutubishe mimea na kuongeza mapato ya kilimo cha umwagiliaji katika kata hii. Na kwa kuleta mbolea hii tunawakopesha mkopo wa mfuko mmoja mmoja na mtalipa ndani ya mwaka mmoja hivyo mna kila sababu ya kuongeza juhudi katika kilimo hicho cha umwagiliaji.

Halmashauri ya Nyasa imedhamiria kuboresha kilimo cha umwagiliaji kwa kutoa mikopo ya pembejeo za kilimo na kuongeza kwa kujenga miundo mbinu ya umwagiliaji. Tayari Wilaya ya Nyasa ina Skimu sita za kilimo cha umwagiliaji ambazo ni Kwambe iliyopo Kata ya Chiwanda, Kimbande-Mbambabay, Nyomboka-Lipingo, Lundo-Lipingo, Nkalachi-Liuli, na Ngingama-Linga.

Announcements

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI WILAYA YA NYASA April 18, 2023
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • TANGAZO la nafasi ya kazi February 03, 2023
  • View All

Latest News

  • Mhandisi Stella Manyanya yatatua kero ya wanafunzi kutembea km 30 kufuata shule ya Sekondari

    June 07, 2023
  • Tunaimani na Serikali, wananchi wa Kata ya Mtipwili na Chiwanda

    June 07, 2023
  • Dc Nyasa atembelea miradi ya Boost awataka mafundi kukamilisha Kwa wakati na ubora

    June 05, 2023
  • Mbunge Manyanya aridhishwa na Kasi ya ukuaji wa Utalii Wilayani Nyasa

    June 05, 2023
  • View All

Video

NYASA yampongeza Rais SAMIA jengo jipya la Utawala
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.