• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

KINGERIKITI AMCOS YATOA MAFUNZO KWA WAKULIMA

Posted on: July 30th, 2020

Chama cha  cha Ushirika cha Msingi cha  Mazao na  Masoko cha Kingerikiti (Amcos),  kwa kushirikiana na Wafadhili wa chama hicho kutoka Nchini Marekani kupitia Shirika la USADF,  Hivi karibuni  Kimetoa Mafunzo kwa wakulima wa kahawa, yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kuzalisha na kuandaa kahawa bora ili kuongeza kipato kwa Mkulima.

Mafunzo hayo ya siku mbili, yametolewa katika Ofisi za Chama, zilizopo Katika Kijiji cha Kingerkiti, Kata ya Kingerikiti Wilaya ya Nyasa, na yametolewa na wakufunzi kutoka Shirika la Sturbucks yenye lengo la kuwafundisha wakulima namna ya kulima, kuitunza na kuandaa kahawa yenye Ubora ili kuifikisha Sokoni.

Akifungua Mafunzo hayo Afisa Ushirika wa Wilaya ya Nyasa Bw.Menance  Ndomba alikipongeza chama hicho kwa kutoa  mafunzo kwa wakulima yatakayowawezesha Wakulima,  kukabiliana na wadudu waharibifu wa zao la kahawa  ambalo pia ni zao la  Kimkakati.

Aidha ametoa Wito kwa wanaushirika kushikamana, ili kuuendeleza Ushirika kwa kuwa ndiyo nguzo pekee kwa Wakulima wa Zao la Kahawa ambayo huwawezesha kuunganisha nguvu zao wakati wakuyafikisha mazao yao sokoni na kuhakikisha chama kinakwenda vizuri kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana hivyo wana kila sababu ya kushikamana.

“Ndugu zangu wanaushirika wa Chama Cha Msingi cha Mazao cha Kingerikiti, Nichukue Fursa hii kuwapongeza Viongozi wa Chama na wafadhili wa Chama hiki, USADF kwa kutoa mafunzo ambayo yanawajengea uwezo wakulima namna ya kulima, kupambana na wadudu waharibifu na kuiandaa kahawa bora itakayo washawishi  wanunuzi, wanunue kahawa iliyokuwa na viwango vinavyokubalika na kwa bei nzuri, Aidha napenda kuwafahamisha rasmi kwamba kufuatia mafunzo haya mmeanzisha rasmi mchakato wakuyafikia masoko maalumu na kwa sasa tunajisajiri SOKO la CAFÉ Practice  Nasema ahsante sana, Nitoe Wito kwa wanachama wa Chama hiki kushirikiana na kuendeleza Ushirika huu kwa kuwa Vyama vingi  vikishapata mafanikio basi kutoelewana kunaanza kwa lengo la kuvuruga Ushirika, ” Alisema Ndomba.

Bw Ndomba aliyataja mafanikio yaliyopatikana Kingerikiti Amcos ni pamoja na kuwa na Mfuko wa Pembejeo wenye thamani ya milioni 38 ambao huwakopesha wakulima pembejeo na kulipa kipindi cha mavuno hali iliyosababisha kuongezeka kwa uzalishaji kutoka tani 10.3 mwaka 2017/2018 hadi kufikia tan 360.34 kwa Msimu wa mwaka 2019/2020. Mafanikio mengine nikukarabati ofisi na kununua vifaa vya ofisi, na kununua Mtambo wa kuchakata kahawa wenye thamani ya miliono 47.

Naye Mkufunzi wa mafunzo hayo  kutoka Shirika la Sturbucks Bi Bahati Mlwilo amesema mafunzo yaliyotolewa kwa wakulima yamewajengea uwezo wa kulima kahawa ya Kisasa, kupambana na Wadudu wanaoharibu kahawa,  namna ya kupambana na magonjwa ya kahawa.lakini pia wamejifunza namna ya kuiandaa na kuifiiksha kahawa yenye ubora na kuongeza kipato kwa kaya na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wao Washiriki wa mafunzo hayo Samweli Kinunda na Severine Mbunda,  waliwapongeza wafadhili pamoja na viongozi wa Chama hicho, kwa kuandaa Mafunzo hayo ambayo yamewasaidia kutambua Changamoto katika zao la kahawa kwa kuwa awali walikuwa wanalima kienyeji na kupata mazao kidogo yasiyo na ubora,  lakini kwa sasa watatumia mafunzo waliyopewa kuboresha na kuitunza kahawa na kuipeleka kiwandani ikiwa na ubora wa hali ya juu ili kujiongezea kipato.

Announcements

  • TANGAZO la nafasi ya kazi February 03, 2023
  • ORODHA ya Watumishi wanaodai malimbikizo ya Mshahara February 08, 2023
  • TANGAZO LA KAZI NYASA DC (MTENDAJI WA KIJIJI) August 18, 2021
  • TANGAZO LA KULIPA KODI YA ARDHI August 30, 2021
  • View All

Latest News

  • MV MBEYA II

    March 23, 2023
  • Wizara ya Afya yatoa mafunzo ya kuzuia na kupambana na magonjwa ya Mlipuko Wilayani Nyasa

    March 21, 2023
  • Nyasa yapewa milioni 800 Hospitali ya Wilaya ya Nyasa.

    March 21, 2023
  • Wananchi Nyasa waishukuru Serikali Kwa kufungua Barabara

    March 17, 2023
  • View All

Video

NYASA yafunguka Kimataifa
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.