• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

NYASA HAIKAMATIKI KIMAENDELEO

Posted on: February 29th, 2020

Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa,  inatarajia kuanza ujenzi wa Kituo cha afya katika Kata ya  Kingerikiti, tarafa ya Mpepo, Kwa Lengo la kutatua kero ya wananchi wa kata hiyo waliokuwa wakisafiri umbari mrefu wa takriban Kilometa arobaini (40), kufuata huduma za matibabu katika Wilaya ya Mbinga.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Nyasa Bw. Jimson Mhagama,  jana wakati akiongea na wananchi wa Kata ya Kingerikiti kwa lengo la kutambulisha mradi na kuwashirikisha Wananchi  ili waweze kushirikiana na Serikali kwa lengo la kutekeleza Mradi huo.

Mhagama alifafanua kuwa, Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa imepokea Shilingi milioni mia mbili tu (Tsh 200,000,000/=) toka Serikali kuu kwa lengo la kujenga kituo cha afya cha Kingerikiti, ili kuwaletea huduma karibu za matibabu kwa wananchi wa kata hiyo, hivyo kwanza kabisa wananchi mnatakiwa kufahamu mradi huu na kushirikiana na Serikali  kuhakikisha ujenzi huu unakamilika ndani ya miezi miwili kuanzia sasa.

Mhagama aliongeza kuwa Serikali imedhamiria kuboresha miundombinu ya Afya katika Wilaya ya Nyasa kwa kuhakikisha inatatua matatizo ya wananchi, hususani kwenye sekta ya afya, kwa kushirikiana na wananchi wa sehemu husika kwa kuangalia jiografia ya Wilaya.

Kwa upande wao Wananchi wa Kata ya Kingerikiti walimpongeza Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli, na Mh. Mbunge wa Jimbo la Nyasa, Mhandisi Stella Manyanya ambaye ni Naibu waziri wa Viwanda na Biashara kwa kutekeleza ahadi yake kwa kuwa aliahidi na ametekeleza ahadi yake ya kuwajengea Kituo cha afya  cha Kingerikiti.

“Sisi wananchi wa Kata ya Kingerikiti,  tumeupokea mradi huu na tunampongeza sana Mbunge wetu na Mh, Rais John Magufuli kwa kutujengea Kituo cha afya katika kata yetu kwa kuwa tulikuwa tunatembea umbali mrefu wa takribani kilometa 40  kufuata huduma za afya katika Hospitali ya Litembo iliyoko wilayani Mbinga au Hospitali ya Wilaya ya Mbinga, hivyo tupewe majukumu yetu na tutahamasishana ili Ujenzi huu utekelezwe kwa muda uliopangwa.” alisema Wiligs ndunguru mkazi wa kijiji cha Kingerikiti kwa niaba ya wananchi wote.

Mganga mkuu wa Wilaya ya Nyasa Dkt Aaron Hyera, aliwaambia wananchi kuwa mara baada ya kukamilika kwa kituo hicho cha afya cha kingerikiti kwa jiografia ya Wilaya ya Nyasa, huduma za afya zitatolewa vizuri kwa kuwa wagonjwa watakuwa hawatembei umbali mrefu na kupata huduma kwa wakati. Aliwataka wananchi hao kushiriki kikamilifu kujenga kituo hicho cha afya ambacho kipo katika Tarafa ya Mpepo na kwa sasa Tarafa ya Mpepo itakuwa na Vituo viwili vya Afya vya Serikali ambavyo ni Liparamba na Kingerikiti.

Aidha uboreshajiwa sekta ya afya katika Wilaya ya Nyasa umeimarika kwa kukamilika kwa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya, iliyojengwa Kijiji cha Nangombo Kata ya Kilosa Tarafa ya Ruhekei na Vituo vya  Afya Kihagara,Mbambabay na Mkili vitafanya idadi ya Vituo Vya Afya kuwa Vitano (05) kitakapokamilika kituo cha Afya cha Kingerikiti.

Imeandaliwa

Na Netho C. Sichali

Kaimu Afisa habari  (W) Nyasa

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wazindua Mtambo wa Hewa Tiba

    May 12, 2025
  • Mwenge wa Uhuru waridhishwa na miradi yote Nyasadc

    May 12, 2025
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Wilayani Nyasa

    May 11, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.