• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

Nyasa yapewa milioni 800 Hospitali ya Wilaya ya Nyasa.

Posted on: March 21st, 2023

SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan  imetoa  shilingi milioni 800 kujenga Hospitali ya wilaya Nyasa,ili kusogeza na kuboresha huduma za afya kwa wananchi ambao awali walilazimika kwenda nje ya wilaya hiyo kufuata matibabu.

Kaimu Mganga mfawidhi wa Hospitali ya wilaya Nyasa Dr Simon Yasin alisema,katika ujenzi huo baadhi ya majengo ikiwemo jengo la wagonjwa wa nje(OPD),wodi ya mama na mtoto na maabara yamekamilika na yameanza kutoa huduma.

Dr Yasin ametaja huduma zilizoanza kutolewa katika Hospitali hiyo ni za wagonjwa wa nje,huduma ya mama na mtoto,kulaza wagonjwa na upasuaji.

“kwa sasa tuko katika awamu ya tatu  na ya mwisho kabisa ya utekelezaji wake,katika awamu hii tunajenga jengo la upasuaji  kwa wanawake na wanaume,jengo la kuhifadhia maiti  sambamba na jengo la dharura ambalo limegharimu shilingi milioni 300”alisema Dkt Yasin.

Kwa mujibu wa Dkt Yasin,majengo hayo yatakapokamilika yatasaidia wananchi wa wilaya hiyo kupata huduma bora za matibabu,kuokoa vifo vya akina wakati na baada ya kujifungua na kupunguza muda wa kwenda maeneo mengine kufuata huduma za afya.

Alisema,Hospitali hiyo ni kubwa na imejengwa eneo ambalo kila mmoja rahisi kufika na imesaidia sana wananchi wa Nyasa kupata huduma za afya karibu.

Dr. Yasini,amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na serikali yake ya awamu ya sita, kwa kuridhia kutoa fedha  zilizotumika katika utekelezaji wa mradi huo muhimu na mkubwa kwa ajili ya wananchi.

Aidha alisema kuwa,kujengwa kwa Hospitali hiyo na kuanza kutoa huduma za matibabu kumewapunguzia wananchi kero  na usumbufu wa kutembea umbali mrefu hadi katika Hospitali nyingine kufuata matibabu.Ametoa wito kwa wananchi,kutumia zahanati,vituo vya afya na Hospitali  zinazojengwa na serikali kwenda kupata huduma za matibabu kwa sababu zimejengwa kwa ajili yao.

Dr Yasin,amewashauri akina mama pindi wanapohisi dalili za ujauzito ni vyema wakawahi kliniki mapema ili kupata ushauri  kwa ajili ya usalama wao na mtoto aliyeko tumboni na wakati na baada ya kujifungua.

Kwa upande wake Muuguzi wa Hospitali Lucia Lagila ametaja faida mojawapo kwa  akina mama kuwahi kliniki ni kupunguza vifo vya mama na mtoto,kupata ushauri wa kitaalam wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua.

Mkazi wa kijiji cha Ng’ombo Blandina Chalima alisema,kujengwa kwa Hospitali hiyo ni ukombozi mkubwa kwao kwani kwa muda mrefu walitegemea kupata huduma za matibabu kwenye zahanati moja tu inayomilikiwa na Kanisa.

Chalima,ameiomba serikali kupitia Halmashauri ya wilaya Nyasa kuhakikisha inapeleka vifaa tiba na  dawa za kutosha  katika Hospitali hiyo,badala ya kuendelea kufuata baadhi ya huduma  katika vituo vingine vilivyopo mbali na makazi yao.Philip  Chambo mkazi wa kijiji cha Kihagala,ameishukuru serikali kuboresha na kumarisha sekta ya afya kwani imesaidia kupunguza vifo vingi  kwa wananchi katika  wilaya hiyo.


Announcements

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI WILAYA YA NYASA April 18, 2023
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • TANGAZO la nafasi ya kazi February 03, 2023
  • View All

Latest News

  • Mhandisi Stella Manyanya yatatua kero ya wanafunzi kutembea km 30 kufuata shule ya Sekondari

    June 07, 2023
  • Tunaimani na Serikali, wananchi wa Kata ya Mtipwili na Chiwanda

    June 07, 2023
  • Dc Nyasa atembelea miradi ya Boost awataka mafundi kukamilisha Kwa wakati na ubora

    June 05, 2023
  • Mbunge Manyanya aridhishwa na Kasi ya ukuaji wa Utalii Wilayani Nyasa

    June 05, 2023
  • View All

Video

NYASA yampongeza Rais SAMIA jengo jipya la Utawala
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.