• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

Rc.Ruvuma afungua nyumba za watumishi shamba la miti Mpepo

Posted on: November 19th, 2022

SERIKALI imetoa zaidi ya shilingi milioni 968 kujenga ofisi na nyumba tatu za watumishi katika shamba la miti Mpepo linalohudumiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)  wilayani Nyasa mkoani Ruvuma.

Akitoa taarifa ya mradi huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mhifadhi Mkuu  wa Shamba la Miti Mpepo John Kimolo amesema mradi wa ujenzi unatekelezwa na Shirika la Nyumba NHC na kwamba jumla ya majengo manne yanajengwa ikiwemo Ofisi kuu ya shamba,nyumba ya Mhifadhi na nyumba mbili za watumishi.

Kimolo amesema serikali inatekeleza mradi huo kwa lengo la kuboresha mazingira bora ya kufanyia kazi na kuishi watumishi wa umma na kwamba mradi umefikia zaidi ya asilimia 95 ya utekelezaji.

“Lengo letu ni kuhamia Mpepo muda wowote,miundombinu ya mtandao wa intaneti na umeme vitakapokamilika kwa sababu shughuli za kiofisi zinahitaji mawasiliano ya mtandao’’,alisisitiza.

Hata hivyo amezitaja changamoto zinazoikabili ofisi hiyo kuwa ni ubovu wa barabara kutoka Nyoni hadi Mpepo inayopitika kwa shida hasa kipindi cha masika,ukosefu wa umeme na moto wa mara kwa mara hasa kipindi cha kiangazi unaosababishwa na wananchi wanapoandaa mashamba yao.

Akizungumza mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi huo,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema serikali kupitia Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Mkoa wa Ruvuma ukiwemo ujenzi wa  ofisi  za kisasa katika shamba la Mpepo.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amewaonya wananchi kuacha kuharibu mazingira kwa kuchoma moto na kuharibu mazingira kwenye vyanzo vya maji ambavyo amesema vinasababisha mabadiliko ya tabianchi.

Amewaagiza viongozi katika ngazi zote kusimamia  na kuunda Kamati za Mazingira kwenye vijiji ili kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayechoma moto misitu na amewataka wananchi kuacha tabia ya kuandaa mashamba kwa kuchoma moto.

“Sisi ndiyo tunaochoma moto na kuharibu vyanzo vya maji,lakini sheria inasema kwenye vyanzo vyote vya maji ndani ya mita 60 hakuna shughuli yeyote ya kibinadamu  inayotakiwa kufanyika,kuanzia sasa ni marufuku kulima au kufanya shughuli zozote kwenye vyanzo vya maji’’,alisisitiza.

Shamba la miti Mpepo ni miongoni mwa mashamba 24 ya miti yanayosimamiwa na kuhudumiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.









Announcements

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI WILAYA YA NYASA April 18, 2023
  • Tangazo la kujiunga na jeshi la kujenga Taifa, (JKT) August 29, 2023
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • NYASA bila ukatili inawezekana

    September 26, 2023
  • Dc Nyasa atembelea miradi ya Afya

    September 25, 2023
  • Kituo Cha Afya Kingerikiti

    September 25, 2023
  • Dc Nyasa apongezwa na wananchi utatuzi wa kero

    September 22, 2023
  • View All

Video

JENGO JIPYA LA UTAWALA NYASADC
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.