• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

RC,Ruvuma aiagiza Wilaya ya Nyasa kubuni vyanzo vipya vya mapato

Posted on: September 21st, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amewaagiza watendaji katika Halmashauri ya Nyasa kuhakikisha wanabuni vyanzo vipya vya mapato ili kuongeza ukusanyaji mapato.

Kanali Thomas ametoa agizo hilo wakati anazungumza na watumishi,madiwani na wazee wa Wilaya ya Nyasa kwenye ukumbi wa chuo cha VETA mjini Mbambabay.

Mkuu wa Mkoa ameitaja wilaya Nyasa kuwa ni moja kati ya Wilaya tajiri mkoani Ruvuma ikiwa na maeneo ya madini ya aina mbalimbali yakiwemo madini ya makaa ya mawe ambayo yanaweza kuingizia wilaya hiyo mapato makubwa kupitia kodi iwapo usimamizi utakuwa wenye tija.

Amesema wilaya ya Nyasa kuanzia mwanzo wa wilaya hadi mwisho ina miamba ambayo ikiwekezwa inaweza kuongeza mapato makubwa katika Halmashauri hiyo.

“Wilaya ya Nyasa ndani ya ziwa Nyasa kuna Samaki wa aina mbalimbali zikiwemo aina 400 za Samaki wa mapambo,wanaovua Samaki hao wananufaika kwa sababu wanauzwa nje kwa Dola,hakikisheni Halmashauri inasimamia mauzo ya Samaki hao ili kuongeza mapato’’,alisisitiza Kanali Thomas.

Katika kuhakikisha mapato yanaongezeka kupitia sekta ya utalii Mkuu wa Mkoa amesema ziwa hilo limebarikiwa kuwa na fukwe zinazofaa kuwekeza ambazo zinavutia kuanzia Chiwindi mpakani na    nchi ya Msumbiji hadi Lituhi mpakani na  wilaya ya Ludewa mkoani Njombe.

Kanali Laban pia ameagiza zoezi la usajiri wa wakulima liendelee ambapo hadi sasa ni wakulima 5000 tu wamesajiriwa katika wilaya ya Nyasa kati ya 16,000.

 Ameagiza kilimo cha Pamoja kipewe kipaumbele ambacho kinawawezesha wakulima wengi kulima zao la aina moja katika sehemu moja.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa amewaagiza ,madiwani katika Halmashauri hiyo kusimamia kikamilifu miradi ya maendeleo ukiwemo mradi wa maji wenye thamani ya shilingi bilioni 4.7 unatekelezwa katika vijiji vya Lituhi na Liuli.

RC Thomas amewaasa watumishi wa umma kuhakikisha wanajenga mahusiano mazuri ili utendaji wao uwe na tija pia amewataka kuacha kujiingiza kwenye madeni mengi yasiyokuwa na tija hali ambayo inashusha ari ya kufanyakazi.

Kuhusu changamoto zinazowakabili wazee zikiwemo za matibabu,ameagiza matibabu ya wazee yatolewe kwa wakati Pamoja na kuendelea kutoa vitambulisho vya matibabu bure kwa wazee,ingawa alitahadharisha kuwa Bima za afya zinazotolewa hazitoshelezi matibabu ya magonjwa yote.

Awali akizungumza kwenye kikao hicho,Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mheshimiwa Aziza Mangasongo alisema hadi sasa wazee waliotambuliwa kwenye wilaya hiyo ni 7528 kati yao waliopewa kadi za afya ni 4020.

Naye Mwenyekiti wa Wazee wa Wilaya ya Nyasa Yustine Mande akizungumza kwenye kikao hicho,amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kusikiliza kero za wazee na kuahidi kuzishughulikia.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma anaendelea na ziara ya kujitambulisha katika Halmashauri zote nane kwa kuzungumza na wazee,watumishi na  waheshimiwa madiwani.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wazindua Mtambo wa Hewa Tiba

    May 12, 2025
  • Mwenge wa Uhuru waridhishwa na miradi yote Nyasadc

    May 12, 2025
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Wilayani Nyasa

    May 11, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.