• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

Tumieni vizuri Raslimali za ziwa Nyasa -Dkt Mpango

Posted on: July 23rd, 2023

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amewaasa wananchi wa Wilaya ya Nyasa kutumia vema rasilimali ya Ziwa Nyasa ambalo lipo katika eneo lao ili kuwa na matumizi endelevu kiuchumi na kijamii.

Makamu wa Rais amesema hayo leo tarehe 23 Julai 2023 wakati akizungumza na wananchi wa Mbambabay akiwa ziarani mkoani Ruvuma. Amesema vitendo vya utupaji taka za plastiki katika ziwa hilo vitaathiri kwa kiasi kikubwa shughuli za uvuvi kwani taka za platiki huchukua miaka mingi zaidi kuoza na kutoweka.

Aidha Makamu wa Rais amewasihi wananchi hao kutunza vyanzo vya maji pamoja na kulinda mazingira kwa jitihada kubwa. Amesema serikali katika mwaka wa fedha 2023-2024 tayari imetenga fedha za ujenzi wa mradi wa umwagiliaji wa Kimbande, Lituhi ,Lundo, na Malini utakaonufaisha wananchi wa Wilaya hiyo.

Vilevile Makamu wa Rais amewahimiza wananchi wa Nyasa kujitokeza na kutumia vema fursa ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaig) iliozinduliwa mkoani Ruvuma ili kupata msaada wa kisheria katika changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo mirathi.

Pia amewataka wananchi wa Mbambabay kulinda amani iliopo nchini kwa kuwa makini na watu wote wanaohatarisha amani wanaoingia kupitia mipaka yae neo hilo. Aidha amewasihi wazazi na walezi kusimamia maadili na uzalendo kwa watoto na vijana ili kuwa na Taifa salama kwa sasa na baadae.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema serikali tayari imetenga shilingi bilioni 22 kujenga Daraja la Mitomoni lilikuwa changamoto kwa muda mrefu iliopelekea wananchi kuzunguka umbali mrefu kufika Makao Makuu ya Mkoa wa Ruvuma. Pia amesema kwa mwaka wa fedha 2023/2024 serikali itaanza utekelezaji wa ujenzi wa Barabara ya Likuyufusi – Mkenda ambapo kwa hatua ya awali ni ujenzi wa kilometa 60 kwa kiwango cha lami Likuyufusi – Muhukulu.

Awali Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ameweka Jiwe la Msingi Mradi wa maji wa Liuli uliopo Kijiji cha Hongi Wilaya ya Nyasa, mradi uliogharimu shilingi bilioni 4.7 unaohudumia vijiji vitano vyenye wakazi 15,823.

Akizungumza mara baada ya kuzindua mradi huo, Makamu wa Rais amewataka wananchi wa eneo hilo kulinda miundombinu ya maji ili iweze kudumu na kutumika kwa muda mrefu. Pia ameagiza ziada ya maji inayopatikana kutokana na mradi huo ambayo imekua ikirudishwa ziwani kutumika katika shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo cha umwagiliaji.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.