• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

WILAYA YA NYASA YAFANYA MAOMBI MAALUM KUMUOMBEA HAYATI DKT MAGUFULI

Posted on: March 25th, 2021

Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma  imefanya maombi maalum, ya Kumuombea aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati  Dkt John Pombe Magufuli, maombi yaliyofanyika katika Viwanja vya Fisheries, Mbamba bay Wilayani Nyasa .

Maombi hayo yamewakutanisha wananchi wa Wilaya ya Nyasa, Waamini wa Dini zote  na Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mh. Isabela Chilumba.

Akihutubia mamia ya wananchi waliohudhuria katika Maombi Maalum,  ya kumuombea Hayati Dkt Magufuli, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa amewataka wananchi wa Wilaya ya Nyasa,  kumuombea kwa sala  Hayati Dkt Magufuli ambaye atazikwa Kesho Wilayani Chato na kumuenzi kwa kuyatekeleza yale yote,  ambayo alikuwa akiyasisitiza yakiwepo kufanya kazi kwa bidii, kwa kuwa hayati magufuli alikuwa ni mchapakazi, na Msimamizi makini wa Shughuli zote, kuanzia Ngazi ya chini ya Kitongoji ,Kijiji hadi Taifa. Hivyo kila mtu amuenzi Hayati Dkt Magufuli  kwa kufanya kazi kazi kwa juhudi na maarifa, na kila mtu kwa nafasi yake ahakikishe anatimiza majukumu yake ipasavyo.

Mh Mkuu wa  Wilaya ameeleza kuwa  wananchi wa Wilaya ya Nyasa wamepokea Taarifa ya kifo cha Hayati Dkt Magufuli kwa Majonzi Makubwa,  kwa kuwa Rais  Magufuli  aliwaahidi wananchi kuja Nyasa,  Kufungua Barabara ya Mbinga Mbamba bay,  iliyojengwa kwa kiwango cha Lami, ambayo Imekamilika na aliahidi kuja kufungua barabara hiyo mwenyewe, alipoweka jiwe la msingi la Barabara  Wilayani Mbinga, na kwa msisitizo Januari 5 mwaka huu, alimtuma Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa kuja kukagua Ujenzi ikiwa ni maandalizi ya yeye kuja kufungua barabara hiyo.

Aidha mh. Chilumba amewataka Wananchi wa Wilaya ya Nyasa kuongeza Mshikamano na Kumuombea Hayati Dkt Magufuli kwa Kuwa Kazi ya Mungu haina makosa, naye kampenda zaidi.

“Ndugu zangu kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya Nyasa, Tumepokea Taarifa ya Kifo cha Hayati Dkt Magufuli kwa Majonzi makubwa, kiasi kwamba mara baada ya kupokea Taarifa Hizi sikuweza kulala kwa kwa kuwa ametutendea mambo makubwa Wilayani Nyasa, na Kuiweka Nyasa katika Ramani ya maendeleo na tulikuwa tukimsubiri aje kutufungulia barabara ya Mbinga Mbamba bay,  iliyojengwa kwa kiwango cha Lami na Imekamilika na kutufanya wakazi wa Nyasa tupate maendeleo Makubwa”.

Mh. Chilumba ameitaja Miradi   Mikubwa  ambayo wananchi wa wilaya ya Nyasa wanamkumbuka Hayati Dkt Magufuli kuwa ni Ujenzi wa Meli za mizigo na Abiria za Ziwa Nyasa,Bandari ya Ndumbi, Hospitali ya Wilaya ya Nyasa,Chuo cha Ufundi Stadi VETA NYASA, Vituo vya afya Mkili, Kingerikiti, Kihagara, Utoaji Elimu Bure na Miradi ya mingine ambayo hawezi kuitaja yote, Umeme,maji na ujenzi wa madarasa katika shule za Msingi na Sekondari Wilayani hapa na kusema kuwa Magufuli aliipenda sana Wilaya ya Nyasa.

Kwa upande wao Viongozi wa Dini ya Kiislam na Kikristo Wilaya ya Nyasa  wamesema wanamuombea Kwa Mungu Hayati   Dkt Magufuli  kwa kuwa alikuwa ni zawadi kutoka kwa Mungu kwa Tanzania na Afrika,  na alifanya kazi kwa nguvu zote na kupiga Vita Rushwa, na ubinafsi na kutumia raslimali za Tanzania kwa manufaa ya Watanzania. Pia wanamuombea Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan hasa katika Kipindi hiki kigumu ili aweze kutekeleza vema majukumu yake ya kulijenga Taifa la Tanzania.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wazindua Mtambo wa Hewa Tiba

    May 12, 2025
  • Mwenge wa Uhuru waridhishwa na miradi yote Nyasadc

    May 12, 2025
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Wilayani Nyasa

    May 11, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.